Posts

Showing posts from December, 2024

BAADHI MAMBO YA KUYAFAHAMU KUHUSU JUA.

Huenda watu wengi hufikiri kwamba wanapoliona jua angani, ndivyo hivyo, na wengine hata hufikiri kwamba ndege hupita inaporuka.  Lakini sivyo ilivyo, jua linazama na kuzama huku likiwa na habari za kushangaza ambazo hata huzifahamu.  Watu wengi huamini kwamba jua huchomoza na kuzama, yaani, mawio na machweo.  Lakini kwa uhalisi inasemekana kwamba jua huchomoza asubuhi na mapema, yaani, ikiwa sayari yetu ya Dunia inageukia upande mwingine wa jua, basi inaonekana katika eneo hilo. Na dunia itakapogeuka na kurudi upande mwingine, giza litaonekana.  Katika makala hii, tunachunguza jua na maelezo yake na jinsi linavyoathiri maisha ya binadamu jinsi Mungu alivyokusudia. Jua ni nini?  Jua lina umbo la mpira, lina haidrojeni na helium, na inakadiriwa na wanasayansi kuwa lilitokea miaka bilioni 4.5 iliyopita.  Na nuru tunayoipata kwenye sayari yetu ya Dunia, ndiyo msingi wa usimamizi wa maisha ya watu, wanyama na viumbe vingine vyote kwenye sayari yetu ya Dunia....

MATUKIO HATARI ZAIDI YA KIKATILI NA KUTISHA

 Tukio la 1 ni “Tate-LaBianca Killings – 1969” Hili tukio linahusisha mauaji ya kinyama ambayo maarufu yanajulikana kama LaBianca Murders.  Haya mauaji yalitokea kati ya Agosti 8 na 10 mwaka 1969. Taarifa rasmi kuhusu kilichotokea zinasema, watu watano waliuliwa vibaya na wanachama wa kundi la "Manson Family."  Lakini kwanza…  Naomba usiwachanganye Freemasons na hii familia ya Manson. Wanaweza kuwa wamefanana ama hawajafanana kimatukio. Huu ukweli hapa tutakuja ujua kwenye Story zinazokuja. Lakini…  Familia ya Manson ni jina tu lililopewa kundi la wahuni waliokuwa wakiishi pamoja chini ya uongozi wa Charles Manson mwishoni mwa miaka ya 60 huko California, Marekani. Kundi hili lilikuwa na mchanganyiko wa vijana ambao ni kama walikua vichaa wanaomuabudu kiongozi wa familia hiyo, bwana Manson.  Manson ambaye historia yake imejaa kumbukumbu za kuingia jela na kutoka. Alisifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi. Na hii ndio sababu alikua na vijana wengi wa...

Unafahamu Faida ya Vitunguu?

Matumizi ya vitunguu maji yanaweza kuwa ya kawaida kwenye mlo wako wa kila siku kutokana na kuwa kivutio kwenye chakula. Mbali na kukiongezea ladha chakula, kitunguu pia ni tiba na kinga nzuri kwenye mwili wa binadamu. Hizi ni faida 10 za kiafya za matumizi ya vitunguu; Kinga ya Magonjwa: Kitunguu kina ‘antioxidant’ nyingi ambayo husaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu. Hii inaweza kusaidia kuzuia magonjwa mbalimbali kama vile saratani, ugonjwa wa moyo na kuzeeka mapema. Hupambana na Bakteria: ‘Allicin’ katika vitunguu zinasaidia utumbo kupambana na bakteria hatari. Ndicho kiambato kinachosababisha harufu kali ya vitunguu na ndiye mpambanaji dhidi ya sumu na magonjwa. Vitamini C: Je, wajua kuwa vitunguu vina kiasi kikubwa cha vitamini C? Vitamini C ni muhimu kwa mwili wako kufanya kazi vizuri. Inasaidia uundaji wa mishipa ya damu na kuboresha mfumo wako wa kinga. Afya ya Mifupa: Kula vitunguu kunaweza kusaidia kuimarisha mifupa na kupunguza hatari ya kuvunjika kwa watu walio ...