MATUKIO HATARI ZAIDI YA KIKATILI NA KUTISHA
Tukio la 1 ni “Tate-LaBianca Killings – 1969”
Hili tukio linahusisha mauaji ya kinyama ambayo maarufu yanajulikana kama LaBianca Murders.
Haya mauaji yalitokea kati ya Agosti 8 na 10 mwaka 1969. Taarifa rasmi kuhusu kilichotokea zinasema, watu watano waliuliwa vibaya na wanachama wa kundi la "Manson Family."
Lakini kwanza…
Naomba usiwachanganye Freemasons na hii familia ya Manson. Wanaweza kuwa wamefanana ama hawajafanana kimatukio. Huu ukweli hapa tutakuja ujua kwenye Story zinazokuja. Lakini…
Familia ya Manson ni jina tu lililopewa kundi la wahuni waliokuwa wakiishi pamoja chini ya uongozi wa Charles Manson mwishoni mwa miaka ya 60 huko California, Marekani. Kundi hili lilikuwa na mchanganyiko wa vijana ambao ni kama walikua vichaa wanaomuabudu kiongozi wa familia hiyo, bwana Manson.
Manson ambaye historia yake imejaa kumbukumbu za kuingia jela na kutoka. Alisifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi. Na hii ndio sababu alikua na vijana wengi waliomfata kila alichosema kama mtume. Lakini usichokijua kuhusu mauaji ya Tate-LaBianca Killings ni kuwa…
Manson na kundi lake wanadaiwa walifanya mauaji yale wakisukumwa na chuki za kikabila. Sasa kama wewe ulidhani ukabila upo kule kwa Wakulima na Wafugaji pekee. Nikwambie tu haya mambo yapo hadi huko uzunguni paliko endelea.
Usiku wa kati ya tarehe 8 na 10, Manson na kundi lake walifanya moja ya matukio mabaya kuwahi kufanywa Marekani. Waliua watu watano wa familia moja. Na ishu haikua kuwaua pekee. Ishu inakuja kwa namna walivyowaua. Wahanga walichinjwa na kukatwa mapanga, huku pia maiti zao zikikutwa na majeraha ya visu maeneo mbalimbali ya miili yao. Lakini hilo halikutosha…
Kwa chuki waliyokuwa nayo Familia ya Manson. Baada ya kufanya mauaji waliandika maneno mbalimbali ukutani, moja wapo likiweno ni neno “Death to Pigs” - kauli ambayo inahusishwa na chuki binafsi ambazo zaweza kuwa ni chuki dhidi ya kabila, dini au rangi. Maneno haya ukutani yaliandikwa kwa damu.
Kwa juhudi za polisi. Manson na wafuasi wake walikamatwa. Manson alipandishwa kizimbani mwaka 1971 ambapo alikutana na adhabu ya kifo. Adhabu ambayo hata hivyo hakuitumikia kwasababu, adhabu hiyo ilibadilishwa kuwa kifungo cha maisha gerezani baada ya Mahakama jimbo la California, Marekani kuifuta adhabu ya kifo mwaka 1972. Manson alifariki mwaka 2017 akiwa na miaka 83. Baadhi ya wafuasi waliokua chini yake bado wako gerezani hadi leo hii.
Mauaji yalofanywa na Familia ya Manson ni moja ya matukio ya kutisha zaidi katika historia ya Marekani na yanaendelea kujadiliwa na kuchunguzwa kutokana na ukatili wake. Haya mauaji hautakiwi kabisa kuyatafuta maudhui yake google. Unaweza poteza kabisa hamu ya kula.
Tukio la 2 ni “Andrei Chikatilo Bodies”
Hili ni neno jingine usilotakiwa kulitafuta kule Google. Neno hilo limebeba maudhui ya maiti za watu waliouliwa na mikono ya Serial Killer mmoja aliyewahi isumbua sana nchi ya Urusi.
Huyu jamaa aliitwa Andrei Chikatilo. Watu wengine bwana sijui huwa wameumbwaje tu. Chikatilo katika maisha yake alifanya mauaji ya watu 50. Lakini tofauti na wale Manson Family - huyu jamaa wengi katika wahanga wake walikua ni wanawake na watoto.
Historia inamjua kama moja ya wauaji katili sana. Chikalito alizaliwa Ukraine mwaka 1936, ambayo kwa wakati huo ilikua ni sehemu ya Umoja wa Kisovieti. Kurasa za historia hazina nakala nyingi zinazoelezea nyakati za furaha katika maisha ya Chikatilo. Huyu jamaa alizaliwa na kukuzwa katika kile kipindi cha njaa kali iliyowahi ikumba nchi ya Urusi. Kuna tetesi ingawa zinafichwa sana, zinadai kuwa…
Miaka ya 1930s wakati Urusi ikipigwa na lile janga la njaa kali kuwahi ikumba nchi hiyo. Inasemekana kuna baadhi ya watu walianza tabia za kula nyama za watu. Wapo walioenda mbali sana na kusema kaka yake Chikatilo alikua moja ya watu waliochinjwa enzi hizo na kuliwa nyama. Hii inatosha kutuambia Chikatilo alitokea katika maisha gani. Lakini…
Wakati wa ujana wake alikua mtu safi tu. Akiwa kijana alihitimu shahada ya ualimu katika chuo cha Rostov. Baadae aliajiriwa kama mwalimu kabla ya kufukuzwa kutokana na matukio yake ya ukatili wa kijinsia. Na kuhusu mauaji yake…
Bado haijulikani kwanini alikua akiua zaidi watoto na wanawake. Taarifa zinasema alikua akitumia vitu vidogovidogo kuwatamanisha wahanga wake. Na kila walipojaa kwenye mfumo… aliwaua vibaya kwa kuwatia vitu vyenye cha kali kwenye miili. Baadhi ya maiti alizibaka huku nyingine zikiwa na ishara za kukeketwa.
Chikatilo hata hivyo alikamatwa mwaka 1990 na alinyongwa mwaka 1994. Picha za matukio yake ni za kutisha na zinajumuisha vitendo vya kikatili kama ubakaji na ukeketaji.
Tukio la 3 ni “Jeffrey Dahmer Killings”
Naomba nikiri kuwa mimi ni moja ya watu ambao tulishindwa kuimaliza tathilia fupi ya Netflix inayoitwa Jeffrey Dahmer. Kama huifahamu…
Hii ni tamthilia inayoeleza historia ya mauaji ya muuaji aliyewahi sumbua Marekani, aliyeitwa Jeffrey Dahmer. Na kama unataka kujua ni kiasi gani baba na mama ni muhimu katika makuzi ya mtoto. Au ni kiasi gani ugomvi wa wazazi unaweza pelekea kuharibu maisha ya mtoto. Naomba itafute hiyo tamthilia ina mafunzo makubwa. Sasa turudi kwenye story yetu. Kwanini hautakiwi kutafuta google neno “Jeffrey Dahmer Killings”
Historia, hasa nchi ya Marekani haimjui Jeffrey Dahmer kama muuaji pekee. Huyu jamaa anajulikana muuaji ambaye alikula pia nyama za wahanga wake. Akiathiriwa sana na ugomvi wa wazazi wake ambao kwa kiasi fulani uliathiri makuzi yake. Dahmer alijikuta anakua muuaji – huku wahanga wake wengi wakiwa ni wavulana na wanaume waliojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Mashoga.
Dahmer aliwalaghai wengi katika wahanga wake kwa gia ya kama anawataka kimapenzi. Na mara baada ya kuingia mtegoni. Aliwapa madawa ambayo aliyachanganya kwenye vinywaji. Baada ya wahanga wake kunywa na kupoteza fahamu. Walishtuka wakiwa kitanzini tayari. Dahmer aliua vibaya. Aliwatesa wahanga wake kwa kuwapiga nyundo na kuwakatakata na vitu vyenye ncha kali.
Jeffery Dahmer aliua na kula nyama za wahanga wake kati ya miaka ya 1978 na 1991. Picha na matukio aliyoyafanya Dahmer ni ya kutisha sana. Alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani mwaka 1992. Lakini mwaka 1994 aliuawa na mfungwa mwenzake akiwa gerezani.
Tukio la 4 ni “Faryion Wardrip Crime Scene”
Huyu ni seria killer mwingine ambaye hautakiwi kabisa kutafuta hata jina lake tu kule Google. Lakini tofauti na Dahmer, huyu jamaa kwanza, wahanga wake walikua ni wanawake pekee wakitajwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25.
Aidha, tofauti na Dahmer, huyu jamaa yeye aliua wanawake 5 tu. Mauaji aliyoyafanya ndani ya miaka miwili – tangu 1984 hadi 1986 kule Texas Marekani. Lakini wakati namba ya mauaji yake ikionekana ni ndogo. Suala halikua kwamba aliua watano tu. Suala zima na msala wote ulikua kwenye namna alivyowaua hao wanawake. Huyu jamaa anaitwa Faryion Wardip. Na yupo hai hadi leo akisubiri kitanzi kule Texas Marekani.
Huyu jamaa alikua anawawinda na kuwaua wanawake katika maeneo ya mbali na makazi. Vitendo vyake vya kinyama vilianzia kwenye kubaka kabla ya kuwaua kikatiki wahanga wake. Faryion alitekeleza mauaji ya kwanza mwaka 1984. Lakini, mwaka 1986, baada ya kutekeleza mauaji yake ya mwisho – alikamatwa na kuhukumiwa miaka 35 gerezani baada ya kukiri kosa hilo.
Faryion alikaa gerezani miaka 11 tu na aliachiwa huru kwa msamaha. Lakini akiwa uraiani. Uchunguzi wa Polisi ulimhusisha na mauaji mengine manne aliyofanya mwaka 1984 na 19885. Alikamatwa tena ambapo pia alikiri. Mara hii alipatiwa hukumu ya kifo.
Huyu jamaa hadi dakika hii yuko jela anakula maharage akisuburi karatasi za kifo chake zisainiwe. Picha za matukio alofanya pia hushauriwi kabisa kuzitafuta, zitakuharibia siku.
Tukio la 5 ni “Jack The Ripper Victims”
.Anaitwa Jack the Ripper. Moja kati ya Serial Killers waliowahi isumbua sana Uingereza mwishoni mwa Karne ya 19. Historia haina mengi ya kuzungumzia kumhusu Ripper kwasababu kwanza hakuwahi kukamatwa wala kujisalimisha.
Kinachofahamiwa ni kuwa. Huyu alikua moja ya wauaji hatari sana kuwahi kutokea. Staili yake ilikua ya tofauti. Ufanano katika namna alivyowakata wahanga wake – uliibua nadharia kadhaa ambazo baadhi zilidai huenda alikua ni mtu alofanya kazi za bucha. Yote kwa yote, licha ya utaftwaji wake kuhusisha wataalamu na wapelelezi waliokuwa miamba karne hiyo, mwamba hakukamatwa.
Richer aliua vibaya na kutenganisha miili ya wahanga wake ambao wengi walikua wanawake. Alizua hofu maeneo mengi kabla ya kutokomea kusikojulikana na kuacha swali ambalo historia imekosa jibu lake hadi leo.
Tukio la 6 ni “Ed Gein Crime Photos”
Hii nikuonye tena. Picha za matukio ya huyu jamaa hazifai. Achana nazo kabisa. Ed Gein Crime Photos ni keyword ambayo imebeba maudhui ya picha za wahanga wa Edward Theodore Gein. Lakini huyu hakuwa mtu wa kawaida tu. Iko hivi:
Jina maarufu anajulikana kama "The Butcher of Plainfield," enzi za uhai wake. Huyu jamaa alikua muuaji. Lakini pia anatajwa kuwa na tabia chafu za kufukua makaburi na kuiba maiti ambazo nitakwambia hapa chini alikua anaenda kuzifanyia nini.
Historia inasema…
Edward alizaliwa Marekani miaka ya mwanzo ya 1900. Kama Jeffrey Dahmer, huyu nae alikua mhanga mkubwa wa matatizo ya kifamilia. Huyu jamaa alitokea kwenye familia ambayo baba alikua mlevi kupita kiasi. Mama yake alikua na tabia mbaya, mkali na hakuna alichomfundisha mwanaye zaidi ya ubaya aliokua nao.
Baada ya kifo cha mama yake. Katikati mwa miaka ya 1940s, Edward alianza matukio ya kutisha ya kufukua na kuiba maiti toka makaburini. Ni kama hakuwa na akili timamu. Na unadhani alikua anazifanyia nini hizo maiti?
Nakala zinasema alikua anatoa vitu katika mifupa na baadhi ya sehemu za mwili kutengeneza mapambo ya nguo. Kuna muda alitengeneza masanamu ya kutisha ambayo aliyapamba na mabaki ya maiti alizochimba makaburini. Haya matukio aliyaanza kabla hajaanza kuua.
Ulipofika mwaka 1954, Edward alifanya mauaji yake ya kwanza baada ya muda mrefu wa kuchimba maiti toka makaburini. Aliendelea na tabia mpya hadi 1957. Lakini hakuna marefu yasiyo na ncha. Alikamatwa… na baada ya taratibu kadhaa za polisi. Ilibainika ni mgonjwa wa akili hivyo hawezi somewa mashtaka. Aliwekwa tu chini ya uangalizi. Na ulipofika mwaka 1964…
Edward… alitangazwa kuwa na akili timamu. Alihukumiwa kifungo gerezani ambako alifariki mwaka 1984 akiwa na miaka 77. Mauaji yake na vitendo vyake vya kinyama vimetoa idea kwa filamu nyingi za kutisha. Picha za matukio yake ni za kutisha na hazifai kuangaliwa.
Tukio la 7 ni “Ted Bundy Crime Photos”
Hizi ni picha za matukio yalofanywa na Theodore Robert Bundy ambaye anajulikana kama moja ya Serial Killer hatari kuwahi kutokea. Kitu cha pekee kwa huyu jamaa ni kuwa, yeye uraibu wake wa kuua uliwahusu wanawake na watoto pekee.
Na kwa kipindi cha miaka 4 yaani tangu 1974 hadi 1978, Ted Bundy aliua takriban wanawake na watoto 30. Hata hivyo, pamoja na Ted kukiri mauaji hayo, idadi kamili ya waliofia mikononi mwake inatajwa huenda ikawa ni kubwa.
Bundy naye alikamatwa mwaka 1989. Baada ya uchunguzi wa hapa na pale na kukiri mauaji 30, alihukumiwa kunyongwa. Picha za matukio alofanya ni vitu hautakiwi hata kuvisikia kwa mbali.
Lakini kabla sijahitimisha…
Matukio yote niliyokuletea leo yanaonyesha upande mweusi wa historia ya binadamu. Picha za matukio haya zinaweza kuwa za kutisha na za kusikitisha sana. Kama una moyo mwepesi, ni bora uepuke kuangalia picha hizi kwenye Google. Kumbuka kuwa baadhi ya mambo ni bora kutosikia wala kuona ili kulinda afya yako ya akili.
Comments
Post a Comment