BILIONEA MDOGO ZAID

 Selena Gomez ambaye ametajwa na kampuni inayotoa habari za kifedha ya Bloomberg kuwa mmoja  mabilonea wenye umri mdogo wanawake, ni msanii maarufu wa muziki na filamu kutoka Marekani. 


Alizaliwa Julai 22, 1992, huko Grand Prairie, Texas. Wazazi wake wana asili ya mchanganyiko. 


Mama yake, Amanda Dawn Cornett, ni Mmarekani mwenye asili ya Kiitaliano. Baba yake, Ricardo Joel Gomez, ana asili ya Kihispania na ni Mmarekani mwenye mizizi ya Mexico. Kwa hivyo, Selena Gomez ana mchanganyiko wa asili ya Kihispania (Mexico) na Kiitaliano kupitia wazazi wake.

Alianza kupata umaarufu akiwa mtoto kupitia kipindi cha televisheni cha Disney Channel kinachoitwa Wizards of Waverly Place (2007-2012), ambacho kilimfanya kuwa staa wa watoto.


Mbali na uigizaji, Selena Gomez pia ni mwimbaji mwenye mafanikio makubwa. Ametoa albamu kadhaa maarufu kama Revival (2015) na Rare (2020). Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni kama "Come & Get It," "Good for You," na "Lose You to Love Me." Gomez pia ni mfanyabiashara, mjasiriamali, na mwanzilishi wa chapa ya urembo iitwayo Rare Beauty.


Pia anajulikana kwa kazi zake za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kuwa balozi wa UNICEF na juhudi zake za kuongeza uelewa kuhusu afya ya akili. Ana wafuasi balaa kwenye page yake ya Instagram.


Comments

Popular posts from this blog

MATUKIO HATARI ZAIDI YA KIKATILI NA KUTISHA

HISTORIA YA PYRAMIDS ZA AFRIKA

Mambo yanayoweza kuboresha mapenzi baina ya wapendanao